
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema maafisa wa juu katika chama tawala cha ZANU-PF walitafuta msaada kwa waganga wa Nigeria ili wamuue.
Mugabe ambaye alitoa madai ya kushangaza wakati akisherehekea miaka 91 ya kuzaliwa kwake yaliyokuwa na sherehe kubwa iliyoandaliwa kwa mtindo wa kijamaa wa chama katika harakati za Februari 21.
Kiongozi huyo mkongwe, ambaye yupo madarakani tangu uhuru wa Zimbabwe 1980, alitimiza miaka 91 Februari 21 na kudai kuwa ameagizwa na Mungu kuongoza daima.
Aliwaambia wanachama kwenye sherehe zilizofanyika kwenye hoteli ya juu katika mji wa Victoria Falla ambapo alimfukuza Makamu wa Rais Joice Mujuru ambaye alidaiwa kuwatumiwa waganga wawili wa Nigeria kupanga njama za kumuua.
Bi Mujuru alifukuzwa pamoja na mawaziri wengine 10 kwa tuhuma za kupanga njama za kumuua Rais Mugabe na kuhusishwa na shughuli za rushwa.
No comments:
Post a Comment